HUDUMA ZETU ZA SACCOS
AKIBA YA KAWAIDA YA KUWEKA PESA NA KUTOA
(DEPOSITS)
- Mwanachama kuweka akiba mara kwa mara
- Kutoa pesa kila mara anapohitaji
- Weka akiba mara kwa mara ikusaide kwa mahitaji y
yako ya kila siku
AKIBA YA LAZIMA (SAVINGS)
- Kila mwezi mwanachama lazima kuweka akiba ya lazima shilingi 10,000/=
- Akiba hii haichukuliwi hadi kujitoa uanachama
- haina ada yeyote
- Husaidia kudhamini mkopo
- Itakua inakupa riba kila mwaka
- Itakusaidia kuondoa usumbufu pale unapotaka kukopa na kudhamini
AKIBA YA MALENGO (SPECIALIZED SAVINGS)
- Kuweka akiba ya muda ya kipindi maalumu kulingana na malengo
yaliyopangwa
- Malengo yanaweza kuwa ya mwaka, miaka au miezi. Mwanachama anapanga
kila mwezi anaweka kiasi kadhaa(mfano 100,000) kwa miezi 12 ili
akalipe ada. Hivyo kwa mwaka ni sh 1,200,000
- Hupata riba mwisho wa kipindi cha kuchukua fedha za kulingana na mkataba
AKIBA YA MALENGO (SPECIALIZED SAVINGS)
- Ni akiba ya muda maalumu, inaanzia miezi 3, miezi 6 miezi 9 au mwaka mmoja na zaidi.
- Kiasi kinavyokua kikubwa na riba ndiyo inavyokua kubwa
HISA (SHARES)
- Hisa ni mtaji wa mwanachama kwenye SACCOS
- Mwanachama anaingia SACCOS kwa hisa kianzio sh. 30,000
- Kisha kukaa ndani ya chama miezi 6mwanachama anapaswa awe na hisa si
chini ya sh150,000
- Mwnachama akikaa zaidi ya mwaka anatakiwa awe na hisa za shilingi zaidi ya 300,000
kama hajawahi kukopa
- Mwanachama anahamasishwa aongeze hisa kidogo kidogo ili aweze kupata gawio zuri kila mwaka
- Angalau kila mwanachama awe na hisa za sh 300,000 baada ya kukaa kwenye chama zaidi ya miaka 2
MIKOPO (LOANS)
- Mikopo inatolewa kwa mwanachama baada ya kukaa kwenye chama miezi 2 baada ya kujiunga
- Mikopo inatolewa kwa awamu kila mkopo mwingine unapoisha
- MMkopo wa kwanza hauzidi shilingi 2,000,000/=/li>
- Ili kukopa mwanachama ahakikishe ana akiba 25% ya kiasi anachokopa na hisa zilizokamilika kwa mujibu wa sheria na masharti ya chama.
- Mkopo wa mishahara akiba ya lazima 10% na hisa zilizokamilika kwa mujibu wa sheria na masharti ya chama.
- Mikopo ya viwanja haina akiba ya lazima/li>
- Marejesho ni kwa mwezi au kwa wiki kwa Boda boda
- Mwanachama anapokopa awe na wadhamini wawili wanaotumia akaunti yao vizuri kwa mujibu wa masharti ya chama na sera zake.
The main objectives of the SACCOS
Why we are different
View Details